26
Aug
Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB) ikiongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wake, Dkt. Josephine Rogate Kimaro tarehe 25.08.2025 katika Ofisi zake zilizopo Madema, Maji House, imekutana na ujumbe kutoka The King’s Foundation na Qatar Foundation katika kikao kilichojadili maeneo ya ushirikiano na kujifunza kuhusu miradi mbalimbali ya kipaumbele ya Serikali inayosimamiwa na ZPDB.
Ujumbe huo uliambatana na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aboud Jumbe, Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na Afisa kutoka Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Habari – ZPDB
Useful Links