Taasisi ya ZPDB imewasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Robo ya kwanza (Julai – Septemba), 2024 mbele ya Kamati ya BLW

01
Dec

Taasisi ya ZPDB imewasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Robo ya kwanza (Julai – Septemba), 2024 mbele ya Kamati ya BLW

Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB) tarehe 12 Novemba, 2024 iliwasilisha taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha robo mwaka kwa mwezi Julai – Septemba, 2024 kwa Kamati ya Kudumu ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu ya Baraza la Wawakilishi, iliyofika Ofisi za ZPDB zilizopo Maji House, Madema mjini Unguja.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa jumla ya miradi 36 ya vipaumbele kupitia sekta za Uchumi wa Buluu, Elimu, Afya, Maji, Kilimo na Maendeleo ya Jamii imefanyiwa ufuatiliaji na Taasisi ya ZPDB. Kazi hiyo ya ufuatiliaji iliyofanywa na ZPDB kwa kushirikiana na  Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuitembelea miradi hiyo ili kujuwa changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi.

Kwa upande wa wajumbe wa kamati hiyo waliitaka taassisi hiyo kusimamia kwa umakini suala la miundombinu kwa watu wenye ulemavu katika miradi inayotekelezwa, ili iwe rafiki kwa watumiaji. Mwenyekiti wa kikao hicho, Mussa Foum akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Machano Othman Saidi, alisema ZPDB ndio wasimamizi wakuu wa miradi ya Serikali hivyo ni vyema kuhakikisha miradi inayojengwa iwe na miundombinu rafiki ya watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Afisi ya Rais – Ikulu, Mhe. Ali Suleiman Mrembo alisema suala la miundombinu kwao ni kipaumbele na watajitahidi kuhakikisha hakuna alieachwa nyuma kwa kisingizio cha miundombinu.

Useful Links