19
May
Taasisi ya ZPDB iliungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wengine wa Kitaifa na wa dini na wengineo pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika kushiriki mazishi ikiwemo kuuaga mwili viwanja vya Kisonge Zanzibar wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bwana Charles Martin Hilary. Ujumbe wa ZPDB uliongozwa na Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wake, Dkt. Josephine Rogate Kimaro. Buriani Charles Hilary. Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Useful Links