22
Apr
Mtendaji Mkuu wa ZPDB, Profesa Mohammed Hafidh Khalfan alitembelewa ofisini na kubadilishana mawazo na Mwanadiplomasia na Balozi wa Tanzania nchini Uswidi (Sweden), Mhe. Mobhare Matinyi.
ZPDB kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imemhakikishia Balozi huyo ushirikiano mkubwa muda wowote kwa maslahi mapana ya Taifa.
Balozi huyo aliteuliwa miezi michache iliyopita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mhe. Matinyi aliwahi kuhudumu kama Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania na pia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.
Balozi huyo Kidiplomasia ni wa daraja la kwanza (Ambassador Extraordinary and Plenipotentiary) na anaiwakilisha Tanzania katika nchi nane (8) katika eneo lake yani multiple accreditation. Safari yake ya kuja Zanzibar ni katika kutekeleza na kukamilisha hatua muhimu ya Kidiplomasia inayoitwa courtesy call kwa lengo la kuaga na kupokea maelekezo na maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ili kuyafanyia kazi katika Kituo chake cha kazi kwa maslahi ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Mwisho baada ya ziara yake katika Ofisi za ZPDB na kupokea zawadi kutoka ZPDB, Balozi Matinyi alielekea Ikulu kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiungana na Mabalozi wenzake (kwa hatua ya courtesy call) wanaoiwakilisha Tanzania nchini Rwanda, Msumbiji na Zimbabwe.
Useful Links