Zanzibar kuimarisha mashirikiano na Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nane

12
Jun

Zanzibar kuimarisha mashirikiano na Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nane

Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB) mnamo tarehe 7 Novemba, 2024 ilikutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika Ofisi zake Mjini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kutangaza mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi mbalimbali ya vipaumbele kupitia Reli ya Standard Gauge  (SGR).

 

Katika mazungumzo hayo, Meneja wa Mawasiliano na Habari wa ZPDB, Bwana Mohamed Mansour alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Bwana Masanja Kadogosa na akaomba kutumika kwa TV zilizopo katika sehemu za kusubiria abiria na zile zilizopo ndani ya Reli ya SGR ili kuweka vipindi na makala mbalimbali zinazoelezea mafanikio ya miradi ya vipaumbele ambazo zinaandaliwa na ZPDB, Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hatua hiyo ni ya kimkakati katika kuhakikisha taarifa za mafanikio ya Serikali zinawafikia wasafiri wa SGR, wananchi wengi na Watanzania kwa ujumla.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TRC aliishukuru ZPDB kwa ziara yake hiyo muhimu na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kasi kubwa ya maendeleo na mafanikio katika utekelezaji wa miradi ambayo imetekelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

 

Kwa ujumla, Mkurugenzi huyo alifurahishwa na mawazo na ubunifu uliokuja nao ZPDB katika kushirikiana na TRC katika kutangaza mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo yeye binafsi na TRC wanakubaliana na wanaunga mkono hatua hiyo kwani Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinatakiwa muda wote zishirikiane katika kuleta maendeleo kwa Watanzania na akasisitiza kuwa makala na vipindi hivyo viwasilishwe TRC na hivyo utekelezaji wa suala hilo hauna mjadala bali unaweza kuanza haraka.

Useful Links